Watumishi wa Umma waaswa kutokuwa na hofu na mfumo mpya wa tathmini ya watumishi.

Na Mwandishi Wetu, MOI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma Mhe: Ridhiwani Kikwete amesema Mfumo Mpya wa Tathimini ya Watumishi wa Umma (SAU) hauna lengo la kumuondoa kazini ama kuwaonea watumishi wa umma hivyo hawana sababu ya kuuhofia mfumo huo.

Mhe: Kikwete amebainisha hayo leo Desemba, 13, 2023 wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa umma kutoka Taasisi ya Tiba ya Mufupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Shirika la Masoko Kariakoo na Bodi ya Sukari Tanzania yaliyofanyika MOI.

Amesema lengo la mfumo huo ni kuiwezesha kupima utendaji wa watumishi wake kwa njia rahisi na kuongeza ufanisi wenye tija kazini.

“Mfumo hauna lengo la kukomoa watu, tutakuwa na utumishi wa umma unaotimiza majukumu, utawezesha kupamga utumishi wenye tija, huna sababu ya kuhofia” amesema Mhe: Kikwete

Aidha aliipongeza MOI kwa kutoa huduma bora kwa Watanzania na kuitaka kuendelea na kasi hiyo kwa maslahi ya umma.

“MOI inaendelea kuwa bora hii yote ni juhudi zako Profesa Makubi na timu yako, hongera sana, tunahitaji utumishi wenye tija” amesema
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi akimkaribisha Naibu Waziri huyo alimpongeza kwa kuitembelea MOI mara kwa mara na kwamba htua hiyo inaongeza ari kwa watumishi kufanya kazi kwa umahiri.

About the Author

You may also like these