TUGHE na Menejimenti MOI wameazimia kuendeleza ushirikiano ili kuboresha huduma na maslahi kwa watumishi.

Na Mwandishi wetu- MOI

Chama cha wafanyakazi wa sekta ya afya Serikalini (TUGHE) tawi la Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kimefanya mkutano mkuu wake wa mwaka kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kujadili maslahi ya wafanyakazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof.Abel Makubi aliyekuwa mgeni maalum wa mkutano huo amekipongeza chama hicho kwa mahusiano mazuri na Menejimenti na kazi nzuri wanayoifanya ya kusimamia wajibu na haki kwa wafanyakazi.

“Mkataba wa hali bora ni muhimu sana ila tuhanitaji kuwajibika kwa kiwango cha juu kabisa katika kutoa huduma kwa wagonjwa wetu …serikali kuu inatupa mishahara hivyo hatuwezi kujilipa motisha bila kwanza kuongeza uwezo wa kuhudumia watu vizuri kwa kuwa mapato yetu yanatoka huko; sasa niwaombe tuhame kwenye mtazamo wa kufanya kazi kwa mazoea kwa kuagalia muda au masaa bali ni kujipima na kulipwa ziada kutokana na wingi na ubora wa huduma tulizowapa Wananchi (matokeo na malengo/targets) kwa siku “amesema Prof. Makubi

Mgeni rasmi wa mkutano huo CDE. Brendan Maro ambaye pia ni Mwenyekiti wa TUGHE mkoa Dar es Salaam ameishukuru taasisi ya MOI kwa kushirikiana na chama cha wafanyakazi TUGHE katika utendaji majukumu ili kusaidia wafanyakazi kuhudumia wananchi kwa kujitoa.

Naye Bw. Revocatus Mwenyekiti wa TUGHE tawi la MOI amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Makubi kwa maboresho makubwa ya utoaji huduma bora katika taasisi hiyo.

Dkt. Paul Ruge ni Katibu wa TUGHE tawi la MOI amesema wataendelea kufanya mikutano na vikao ili kutatua changamoto za wafanyakazi na mwajiri ili kuongeza ufanisi sehemu ya kazi.

About the Author

You may also like these