Raia wa comoro akoshwa na huduma bora za matibabu MOI

Na Erick Dilli-MOI

Raia wa Comoro aliyepatiwa matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Nuru Abdereman ameelezea kufurahishaa na ubora wa matibabu aliyoyapata kutoka kwa madaktari bingwa na wabobezi wa Taasisi hiyo.

Bi. Nuru amesema kuwa aliteleza kwenye ngazi akiwa nyumbani kwake Comoro na kusababisha maumivu makali kwenye mkono wake.

“Nashukuru mkono wangu umekuwa sawa, nashukuru wafanyakazi wa MOI, madaktari na watu wote Mungu atawalipa, nashukuru kwa huduma zao zote, nafurahi nimepata ndugu na marafiki, nimeona kama nipo nyumbani, hata yale maumivu yameondoka yote”. Amesema Bi Nuru

Amesema kuwa uamuzi wake wa kutoka Comoro kuja Tanzania kutibiwa katika taasisi ya MOI ulikuwa rahisi kutokana na mahusiano mazuri baina ya nchi hizo mbili.

About the Author

You may also like these