MOI kuweka vitanda vipya na vya kisasa wodini ili kuboresha huduma kwa wagonjwa

Na Amani Nsello-MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) inatarajia kubadilisha vitanda vya wagonjwa katika wodi zake zote ili kuendelea kuboresha huduma kwa wagonjwa wa ndani wanaopatiwa matibabu katika taasisi hiyo.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa, Septemba 20, 2024 na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Mifupa  MOI Dkt. Anthony Assey wakati wa zoezi la kusikiliza maoni, ushauri, changamoto na pongezi kutoka kwa wagonjwa na ndugu wa wagonjwa.

Dkt. Anthony amesema kuwa vitanda hivyo vya kisasa zaidi ya 362 vimeagizwa na hivi karibuni vitafika Tanzania na vinatarajiwa kuwekwa katika wodi zote zilizopo katika taasisi ya MOI.

“Ni kweli vitanda vilivyopo kwa sasa vimechakaa, vimeshatumika zaidi ya miaka 8, katika hilo taasisi ya MOI tumeshalifanyia kazi na niwahakikishie kuwa tumeshaagiza vitanda vya kisasa zaidi ya 362, na muda si mrefu vitafika Tanzania.

About the Author

You may also like these