Wananchi waishauri MOI kujenga eneo la ndugu wa wagonjwa wa mikoani kufikia


NA Abdallah Nassoro-MOI
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imesema imeyapokea na kuahidi kuyafanyia kazi maoni ya ndugu wa wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo kutoka mikoani waliopendekeza kuwapo kwa jengo kwa ajili yao kuishi wakati wakiendelea kuwahudumia wagonjwa wao.

Hayo yamebainshwa leo Aprili 24, 2024 na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Marry Kayola wakati ajibu hoja mbalimbali za wateja wa MOI katika zoezi la kusikiliza maoni ili kuboresha huduma kwa wateja.

Amesema taasisi hiyo imepokea maoni hayo na kwamba itashirikisha taasisi zingine zilizopo katika eneo hilo na kuona ni kwa namna gani wanaweza kutekeleza ushauri wao.

“Tumelipokea na tutalifanyia kazi suala la kulala ndugu wa wagonjwa wanaotoka mikoani, tutashirikisha taasisi zingine za serikali zilizopo eneo hili na tuone njia bora ya kulifanikisha hilo”

Kwa upande wake Daudi Mwegalawa ndugu wa mgonjwa aliyelazwa kutoka mkoani Dodoma amesema licha ya kukabiliwa na mazingira makugu ya kifedha ya kuwahudumia wagonjwa wao, kukosekana kwa eneo la wao kufikia na kuishi limekuwa tatizo linaloongeza gharama za matibabu kwao.

“Ukienda baadhi ya hospitali hasa zile za mishenari utakuta wametenga eneo kwa ajili ya ndugu wa wagonjwa kulala, sijui inashindikanaje kwa hizi za serikali” amesema Mwegalawa na kuongeza kuwa
“Hii ni hospitali ya Taifa kwa maana hospitali zote za mikoani zikishindwa kumtibia mgonjwa analetwa hapa sasa unapokuja hapa unakutana na changamoto ya wewe muuguzi huna pa kulala, sasa niombe serikali iliangalie hili hata kwa siku za usoni”
Kwa upande wake Meneja Mapato wa MOI, amewashauri wagonjwa kujiunga na bima ya afya ili waweze kumudu gharama za matibabu pindi wanapougua.

Naye wa Ubongo Mgongo na Mishipa ya Fahamu Dkt. Mansour Shabani amesema ni jambo la kawaida kwa wagonjwa kurudia vipimo mara kwa mara ili kufahamu maendeleo ya mgonjwa husika.

“Tunaweza kufanya vipimo mara kwa mara ili kujua maendeleo ya mgonjwa, kwahiyo CT scan na hata X-Ray huwa vinarudiwa rudiwa kwa lengo la kujua maendeleo yake” amesema Dkt. Shabani akijibia hoja ya ndugu wa mgnjwa aliyetaka kujua kwanini vipimo vya CT Scan vinarudiwa rudiwa.

About the Author

You may also like these