KOICA yaunga mkono jitihada za MOI katika kuboresha huduma kwa wagonjwa.

Na Mwandishi wetu- MOI


Taasisi ya tiba ya mifupa na ubongo Muhimbili (MOI) leo imepokea msaada wa vifaa tiba wenye thamani ya milioni 25 ikiwemo mashine ya kuvutia uchafu kutoka kwenye kinywa cha mgonjwa asjiyejiweza, stethoscope, kipimajoto cha kidijitali na kitabu cha mwongozo cha ICU kwa wauguzi kutoka Shirika la Ushirikiano la Kimataifa la Korea (KOICA).

Akiongea wakati wa hafla fupi ya kupokea vifaa tiba hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi amesema kwa niaba ya Menejimenti ya MOI analishukuru Shirika la KOICA kwa msaada huo unaenda kuleta tija kwa wananchi wanaopata huduma MOI.

“ Kwa niaba ya Menejimenti ya MOI napenda kulishukuru Shirika la KOICA kwa kutupatia msaada wa vifaa tiba ikiwemo mashine ya kuvutia uchafu kutoka kwenye kinywa cha mgonjwa asjiyejiweza, stethoscope, kipimajoto cha kidijitali na kitabu cha mwongozo cha ICU kwa wauguzi ambavyo vinaaenda kuboresha zaidi huduma bora kwa wananchi….. kwa nafasi ya kipekee namshukuru Esther Choi kwa kujitolea hapa MOI kwa muda wa miezi 11, amekuwa wamuhimu sana katika kutoa mafunzo kwa wauguzi wenzake jinsi ya kuhudumia wagonjwa katika hali tofauti” amesema Prof. Makubi

Aidha Prof. Mkaubi ameipongeza Serikali ya Korea kwa kuzidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuendelea kuboresha sekta ya Afya nchini na anapenda kuona ushirikiano huo unazidi kundelea kati ya Taasisi ya MOI na Taasisi nyingine kutoka nchini Korea.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Nchi – KOICA Manshik Shin amesema wataendelea kushirikiana na MOI katika nyezo mbalimbali kwa kuendelea kuleta wataalam mbalimbali wa Afya kutoka nchini Korea kuja MOI kwaajili ya kubadilishana uzoefu na kuzidi kuboresha huduma za afya hapa nchini

Naye, Muuguzi kutoka Korea Esther Choi ameushukuru Uongozi na wafanyakazi wa MOI kwa kumpa ushirikiano mzuri katika kipindi chote alichojitolea kwenye utoaji wa huduma za uuguzi na kufanya warsha na mafunzo mbalimbali muhimu kwa kitengo cha wagonjwa mahaututi (ICU) katika Taasisi ya MOI

Mkurugenzi wa huduma za uuguzi – MOI Fidelis Minja amesema kwa muda wa miezi 11 ya Esther amefanya makubwa katika kushirikiana na kuwasiliani na wenzake na Wauguzi wote kutoka MOI wamejifunza mengi kutoka kwake ambayo yataazidi kuboresha utoaji huduma bora kwa wananchi.

About the Author

You may also like these