Na Mwandishi wetu -MOI
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe.Balozi David Concar ametembelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili MOI na kukutana na menejimenti kwa lengo la kuainisha maeneo ya kimkakati ya kudumisha ushirikiano kati ya MOI na taasisi za nchini Uingereza.
Katika ziara hiyo Mhe Balozi . David Concar alipokelewa na Menejimenti ya MOI ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Prof.Abel Makubi.
Mhe. Balozi Concar ameipongeza taasisi ya MOI kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa na kuahidi kuudumisha ushirikiano uliopo kati ya MOI na uingereza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi amesema Taasisi ya MOI inatoa huduma bingwa na kibobezi za Mifupa,Ubongo na Mishipa ya Fahamu hapa nchini na kutoa mafunzo kwa wataalamu kutoa Afrika Mashariki kati na Kusini.
“Mhe Balozi tunashukuru sana kwani nchi yako imekua ikiungana nasi mara kwa mara katika kubadilishana ujuzi pamoja na masada wa vifaa tiba na vipandikizi”
amesema Prof.Makubi.
Ushirikiano baina ya MOI na uingereza utajikita katika maeno ya utafiti, tiba, mafunzo, kubadilishana uzoefu na upatikanaji wa vifaa tiba.