Wananchi waendelea kujitokeza kupata huduma katika banda la MOI SABASABA.



Na Abdallah Nassoro-Sabasaba

Wananchi mbalimbali wameendelea kujitokeaza kupata huduma za ushauri wa matibabu katika banda la Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) katika maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yaliyoanza Mei, 28 2024 jijini Dare salaam.

Banda la taasisi ya MOI linapatikana jengo la China Pavilion, chumba namba 15,16,17 ambapo huduma za ushauri wa matibabu ya mifupa, ubongo, mishipa ya fahamu, tiba lishe na huduma za viungo saidizi (bandia) na mazoezi tiba zinatolewa bure.

Meneja Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi amesema ushiriki huo ni sehemu ya kusogeza huduma za MOI karibu na wananchi na ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutembelea banda hilo kwa ajili ya kupata ushauri wa kitabibu bure.

About the Author

You may also like these