Wagonjwa 300 wahudumiwa banda la MOI maonesho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza

NA Mwandishi Wetu-MOI

Jumla ya Wagonjwa 300 wamehudumiwa katika banda la Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) katika maonesho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza yaliyofungwa leo Novemba 18, 2023 katika viwanjwa vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Afisa Muuguzi daraja la kwanza wa MOI, Tupilike Mwakamyanda amesema wagonjwa wengi waliohudumiwa katika banda hilo wanamatatizo ya mgongo, kiungo na maungio.

Amesema mbali na ushauri, uchunguzi na tiba pia wapo wagonjwa walioandikiwa rufaa kwajili ya kufanya uchunguzi wa kina na matibabu MOI.

“Huduma hizi zilikuwa zinatolewa bure, ambapo tumefanikiwa kuwatibu wagonjwa 3000 wastani wa wagonjwa 60 kwa siku…kati ya hao wanawake 167 na wanaume 133” amesema Tupilike

Maonesho hayo ya siku tano yamefikia kilele chake leo Novemba 18 2023 yakifungwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

About the Author

You may also like these