MOI iendelee kushirikiana na wadau wengine kupunguza ajali za boda boda.

Na Mwandishi wetu -MOI

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameishauri Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) iendelee kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ili kutoa mafunzo shirikishi na Bodaboda kwa ajili ya kupunguza ajali.

Naibu Waziri Dkt. Mollel ametoka ushauri huo leo Novemba 18, 2023 alipotembelea Banda la MOI katika kilele cha wiki ya magonjwa yasiyoambukiza yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mollel ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema ni vizuri kwa taasisi hiyo kushirikiana na taasisi zingine zinazojihusisha na udhibiti wa ajali ili kutoa elimu kwa vijana na wanafunzi shuleni.

“Mshirikiane na taasisi zingine mtoe semina kwa vijana na wanafunzi shuleni ili kupunguza ajali za barabarani…kazi kubwa mnafanya kuduhumia wagonjwa lakini ni muhimu tuwekeze kwenye kudhibiti” amesema Dkt. Mollel

Awali Mkuu wa Kitengo Cha Takwimu Cha MOI Dkt. Joel Gwemelo alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa asilimia 35 hadi 40 ya wagonjwa wanaopokelewa MOI wanaopata ajali zinasababishwa na bodaboda.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi amesema taasisi yake imepiga hatua kubwa katika kuboresha utoaji huduma ikiwa pamoja na uanzishwaji wa klinik mpya ya wagonjwa maalum na kutoka nje na nchi.

“Rufaa nyingi za nje haziendi zinaishia hapahapa kwa sababu serikali imewekeza kwenye taaluma kwa madaktari wetu na vifaa vya kisasa…tuna madaktari washauri waelekezi ambao wamebobea katika upasuaji wa tiba ya mifupa, ubongo, tuna wataalam wa kutosha na waliobobea” Prof Makubi na kuongeza kuwa

Tuna vifaa vya kisasa kabisa tunaweza kufanya operehseni nyingi bila taha kufungua na kupunguza muda wa mgonjwa kukaa wodini na kupona haraka na kwa gharama ndogo”

About the Author

You may also like these