MOI ina wataalam wakutosha na vifaa tiba vya kisasa kutoa huduma kimataifa

Na Mwandishi Wetu-MOI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) Prof. Abel Makubi amesema taasisi yake imejitosheleza kwa kuwa na wataalam wabobezi wa upasuaji wa mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu pamoja na vifaa tiba vya kisasa kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi ndani nan je ya nchi.

Akizungumza na mwandishi wa habari leo Novemba 18, 2023 katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza yaliyofanyika Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Prof. Makubi amesema serikali imesomesha wataalam wabobezi wa kutosha na vifaa tiba vya kisasa ili kuboresha tiba na kupunguza wangonjwa wanaoenda kutibiwa nje ya nchi.

“Rufaa nyingi za nje haziendi zinaishia hapahapa kwa sababu serikali imewekeza kwenye taaluma kwa madaktari wetu na vifaa vya kisasa…tuna madaktari washauri waelekezi ambao wamebobea katika upasuaji wa tiba ya mifupa, ubongo…tuna wataalam wa kutosha na waliobobea” Prof Makubi na kuongeza kuwa

Tuna vifaa vya kisasa kabisa tunaweza kufanya operehseni nyingi bila hata kufungua na kupunguza muda wa mgonjwa kukaa wodini na kupona haraka na kwa gharama ndogo…kwa sasa hivi tumepanua kwa kuweka dawati la wagonjwa wa nje na wenye uwezo wa kulipia ili mtu apate huduma kwa haraka” Prof. Abel Makubi Mkurugenzi Mtendaji MOI

About the Author

You may also like these