Wagonjwa 85 wahudumiwa banda la MOI maonesho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza.

NA Mwandishi Wetu-MOI

Wagonjwa 85 wamehudumiwa katika banda la Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) katika maonesho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza yaliyoanza jana Novemba 14, 2023 katika viwanjwa vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Kati ya wagonjwa hao 25 walihudumiwa siku ya kwanza ambayo ni jana na 60 wamehudumiwa leo na kufanya jumla ya wagonjwa wote waliohudumiwa ndani ya siku mbili hizo kufikia 85.

Maonesho hayo yanaendelea hadi Jumamosi Novemba 18, 2023 yatakapofungwa na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa

Huduma katika maonesho hayo ni bure ambapo wagonjwa wanatapa huduma za uchunguzi, ushauri na tiba

About the Author

You may also like these