Na Stanley Mwalongo- MOI
Fundi Sanifu vifaa tiba wa Taasisi ya tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Jared Elly Ahago ameshinda zawadi ya Millioni 5 kwa kubuni mashine maalum inayoboresha usalama wa mgonjwa anayefanyiwa upasuaji na Urahisi kwa daktari (A designed automatic Suction machine )
Zawadi hiyo alikabidhiwa jana Oktoba 03, 2024 katika kongamano la 11 wadau wa sekta ya afya (Tanzania health summit) liliofanyika Fumba town, Zanzibar na Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui.
Mhe. Mazrui aliwapongeza wabunifu wote waliofika hatua ya Tatu bora na kuhimiza Ubunifu zaidi kuendelea kufanyika kwa ajili ya kukuza Sekta ya Afya na utoaji huduma kwa wananchi.
Naye Ahago amewashukuru waratibu wa kongamano hilo kwa kupatiwa zawadi hiyo na kusema mashine hiyo amebuniwa kwa ajili ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji kwa kuongeza usalama kwao wakati wa upasuaji na kumrahishia Daktari kazi ya Upasuaji
“Ubunifu huu ni sehemu ya kuhakikisha huduma za MOI zinazidi kuwa bora zaidi na kuleta tija kwa wananchi wanaokuja kupata huduma mbalimbali na ndio maana nimebuni mashine hii inayaboresha usalama wa mgonjwa anapopata matibabu MOI” Amesema Ahago