MOI yashiriki maonesho wiki ya magonjwa yasiyoambukiza.

Na Mwandishi Wetu-MOI

Taaasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) inashiriki katika maonesho ya maazimisho ya wiki ya kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Katika banda namba Nane MOI wanatoa huduma za ushauri, matibabu na uchunguzi kwa magonjwa ya Mifupa, ubongo, mishipa ya fahamu, viungo bandia, huduma za kupima uzito, urefu na BMI bure bila malipo yeyote.

Mgeni wa heshima Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ametembelea banda la MOI na kupongeza jitihada zinazofanywa katika kuwahudumia wagonjwa.

Maonesho hayo yataendelea hadi Jumamosi Novemba, 18, 2023 ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.

About the Author

You may also like these