Mafunzo ya kimataifa upasuaji wa vichwa na mishipa kufanyika MOI

Taasisi ya tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kuanzia tarehe 20-24/11/2023 inatarajia kuendesha mafunzo ya kimataifa kuhusu ubobezi katika Upasuaji wa Vichwa na Mishipa.

Mafunzo hayo yameandaliwa na MOI kwa kushirikiana na chama cha madaktari wa upasuaji wa Ubongo , vichwa , mgongo na mishipa kutoka Ulaya ‘Europen asociation of Neurosurgical Societies’ (EANS).

Mafunzo hayo ya siku 5 yatafanyika katika hapa Tanzania (MOI) ambapo madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo , mishipa na mgongo, fellows, residents, madaktari wa dawa za usingizi na ganzi kutoka mikoa na mataifa mbalimbali watashiriki.

Mafunzo haya ambayo ni ya kwanza Afrika Mashariki kufanywa pamoja na EANS, yatawajengea uwezo watalaamu hawa kufanya upasuaji wa kisasa zaidi.

About the Author

You may also like these