Madaktari bingwa wabobezi wa upasuaji wa ubongo kutoka mataifa 12 duniani wapiga kambi MOI

Na Mwandishi Wetu-MOI

Madaktari bingwa wabobezi wa upasuaji wa Ubongo na mishipa ya fahamu kutoka nchi 12 duaniani wameweka kambi ya siku tano katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) ili kubadilishana ujuzi, maarifa na uzoefu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya MOI ya kuifanya kitovu cha umahiri katika elimu na mafunzo ya tiba barani Africa.

Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Novemba 20, 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi ambaye amesisitiza kuwa taasisi yake imeandaa mafunzo hayo kwa kushirikiana na Umoja wa Madaktari wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu Ulaya (EANS) kwa lengo la kubadilishana uzoefu na ujuzi na washiriki wa mafunzo hayo.

“Mafunzo haya yanaakisi dhamira ya taasisi yetu kujikita katika umahiri wa kutoa elimu na mafunzo ikiwa ni sehemu ya mipango yetu … kwa kuandaa tukio hili tunawekeza katika huduma bora za afya kwa Tanzania ya sasa na badaye” amesema Prof. Makubi

Mkurugenzi wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya fahamu MOI Dkt. Limery Mchome amesema mafunzo hayo ya siku tano kuanzia Novemba 20 hadi 24, 2023 yameshirikisha wataalam kutoka nchi za Austria, Norway, Sweden, USA, Urusi, India, Jamhuri ya Czech, kenya, Malawi, Zambia, Uganda na wenyeji Tanzania kwa lengo ni kubadilishana ujuzi na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma bora za kibobevu katika matibabu ya upasuaji kupitia kwenye fuvu na e matundu ya pua bila kufungua fuvu lakini.

“Kuna kozi maalum ya matibabu ya stroke ambapo iwapo mgonjwa akiwahishwa hospitali ndani ya mda mfupi tangu apate stroke anaweza kupata matibabu hayo bila kufungua fuvu…katika kambi hii tuna mafunzo ya kufanya operation kwa kutumia darubini rahisi ambapo itawawezesha madaktari waliopo katika hospitali zisizokuwa na darubini maalum ya kufanyia upasuaji pia kuweza kufanya upasuaji huo ukiwa na matokeo mazuri”, amesema Dkt. Limery.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya kimataifa ya kamati ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu Jumuiya ya Ulaya (EANS) Dkt. Ondra Petr amasema watajikita zaidi kwenye mafunzo kwa vitendo ili kurahisisha uhamishaji wa teknolojia kwa wataalam.

About the Author

You may also like these