Balozi wa Japan nchini Tanzania atembelea MOI

Na Mwandishi Wetu-MOI

Balozi wa Japani nchini Tanzania Yasushi Misawa ametembelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) na kufanya mazungumzo na menejimenti ambapo ameahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za afya ndani ya taasisi hiyo.

Mapema leo Novemba 21, 2023 saa 6:00 mchana balozi Misawa aliwasili MOI na kupokelewa na Menejitimenti ikiongonzwa na Mkurugenzi Mtendaji Prof. Abel Makubi ambaye aliishukuru serikali ya Japan kwa kusaidia kusomesha madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu wawili ambao wamekuwa msaada mkubwa kwa taasisi.

“Tunaye madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu wawili ambao wamesomea nchini Japan…tunashukuru kwa jitihada hizo kwani wakati anasomeshwa huyu wa kwanza Tanzania ilikuwa na madaktari wawili tu wa upasuaji wa ubongo lakini kupitia wao kwasasa hapa MOI tuna madaktari 10”

Daktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu Dkt. Hamis Shaban amesema pamoja na mafanikio makubwa ambayo taasisi imeyafikia bado jitihada zinahitajika kuwekeza katika kuboresha huduma kwa wataalam wengi kuongeza ujuzi kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Balozi Misawa amebainisha kuwa serikali ya nchi yake ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika sekta ya afya ikiwa pamoja na kutoa udhamini wa masomo kwa madaktari ili kuisaidia kufikia lengo la kutoa huduma bora za afya nchini.

About the Author

You may also like these