MOI yashiriki zoezi la upimaji wa afya bila malipo (Afya check) kwa Mkoa wa Dar es Salaam.


Abdulaziz Seif -MOI

Madakatari bingwa wa upasuaji wa mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kutoka Taasisi ya MOI wameshiriki kwenye zoezi la upimaji wa afya bila malipo (AFYA CHECK) linalofanyika katika Mkoa wa Dar es Salaam kuanzia leo tarehe 20 mpaka 30 Juni 2024 katika viwanja vya Barafu-Mburahati.
Zoezi hilo limefunguliwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Dkt. Toba Nguvula ambaye amewaomba wakazi wa Dar es Salaam na mikoa jirani kuchangamkia fursa ya kupata huduma za kibingwa bure.
“Nawaomba wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili la upimaji afya kwani ni bure kabisa, pia kwa wale wenye matatizo mbalimbali ya mifupa na Mishipa ya fahamu Taasisi ya MOI ipo leo na itaendelea kuwepo kwa siku nyingine tisa zijazo”
“Kutakuwa na utoaji wa huduma hii kwa wilaya zote tano za mkoa wa Dar es Salaam kila wilaya huduma zitakuwepo kwa siku mbili” amesema Mhe. Toba Nguvula.
Naye, mratibu wa zoezi la AFYA CHECK Dr. Isaac Maro ametoa shukrani kwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuunga mkono zoezi la upimaji wa afya kwa wananchi wake
“Natoa shukurani kwa Mhe Rais Dr. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila kwa kuendelea kuunga mkono zoezi la upimaji wa afya kwa wananchi wake ambapo mwaka huu ni mara ya nne tangu tuanzishe huduma hii” amesema Dkt. Maro
Kwa upande wake Daktari bingwa wa mifupa kwa watoto wa MOI Dkt. Bryson Mcharo amewaomba wananchi wajitokeza kwa wingi kupata matibabu bure ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili ( MOI) inaendelea kutekeleza kwa vitendo maono ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kupanua wigo wa huduma za kibingwa karibu na wananchi walipo.

About the Author

You may also like these