MOI yapiga kambi ya matibabu kibingwa na kibobezi ya mifupa, mazoezi tiba, ubongo na mishipa ya fahamu kituo cha afya Bunju A


Na Abdallah Nassoro- Bunju ‘A’

Madaktari bingwa wa tiba ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kutoka Taasisi ya MOI wamepiga kambi ya siku tatu ya matibabu ya kibingwa na kibobezi katika kituo cha Afya cha Bunju ‘A’ Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kambi hiyo imeanza leo Alhamisi tarehe 20 na itaendelea hadi Jumamosi tarehe 22 Juni, 2024 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa taasisi wa kusogeza huduma za kibingwa na kibobezi karibu na wananchi.

Katika kambi hiyo huduma za matibabu ya mifupa, ubongo, mishipa ya fahamu na mazoezi tiba (Fiziotherapia) zinazotolewa kwa gharama nafuu.

Wananchi wote wenye matatizo ya mifupa ikiwa pamoja na kupinda kwa mifupa, mivunjiko, kupoteza mguu, mkono, maumivu ya mgongo, kiuno, magoti, ubongo na mishipa ya fahamu wafike kituoni hapo kwa matibabu

About the Author

You may also like these