Dkt. Lemeri awapa elimu ya afya wakazi wa Arusha


Na Stanley Mwalongo- Arusha

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya tiba ya mifupa na ubongo Muhimbili (MOI) Dkt. Lemeri Mchome ametoa elimu juu ya Afya ya namna bora ya kujikinga na magonjwa ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kwa wananchi waliojitokeza katika kambi ya matibabu iliyoandaliwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda.

Dkt. Mchome ametoa elimu hiyo leo Juni 26, 2024 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo amewashauri wananchi jinsi ya kujikinga, kujilinda dhidi ya magonjwa mbalimbali yanayotibiwa katika Taasisi ya MOI.

“ Naomba nitumie fursa hii kuwashauri wananchi wenzangu kwamba ni muhimu kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi, kufuata misingi ya lishe bora na kuwa na utamaduni wa kufuatilia mienenendo ya Afya zetu “amesema Dkt. Mchome.

Ushauri wa Dkt. Mchome unakwemda sambamba na agizo Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa la kuhamasisha jamii kushiriki kwenye mazoezi ili kujiepusha na magonjwa yasioambukiza.

Pia, Dkt. Mchome ametoa rai kwa wakazi wa mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa ya kambi hii kupata huduma za madaktari bingwa.
Kwa upande wake Bw. Elisha Makundi ameishukuru ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kuratibu kambi hiyo ya madaktari bingwa na bobezi mkoani Arusha ambayo ilianza Juni 24, 2024 mpaka Juni 30, 2024.

About the Author

You may also like these