Wadau wachangia viti mwendo (Wheelchairs) katika Taasisi ya MOI

Na Mwanidshi Wetu MOI, Jumanne Oktoba 17, 2023

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imepokea viti mwendo (wheelchairs) 10 na tolori moja kutoka taasisi ya upimaji afya shuleni Stufit wenye thamani ya zaidi ya milioni 3.

Akipokea viti mwendo hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi ameishukuru taasisi hiyo na kuongeza kuwa utakwenda kupunguza changamoto ya viti mwendo kwa wagonjwa hospitalini hapo.

“Sisi kama MOI tumekuwa tukishirikiana nanyi kwa mda mrefu na kwamba huu ni muendelezo, sisi menejimenti tunashukuru kwa sapoti hii na itaenda kupunguza changamaoto kwa wagonjwa wenye uhitaji wa viti mwendo” amesema Prof.Makubi

Awali akikabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Stufit, Abbas Surani amesema msaada huo umelenga kupunguza changamoto za uhaba wa viti kwendo kwa wagonjwa wanaoshindwa kutembea wenyewe.

“Taasisi ya Stufit imetoa msaada huu wa viti mwendo 10 na Toroli moja wenye thamani ya sh. 3 milionni ili kusaidia wangonjwa wenye uhitaji…ni imani yetu kuwa msaada huu utapunguza changamoto ya uchache wa viti hivyo” alisema Surani

About the Author

You may also like these