MOI na Global Medcare wajadili kukuza utalii tiba.

Na Mwandishi Wetu, MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imefanya kikao cha pamoja na Taasisi ya Global Medcare kujadiliana juu ya namna bora ya kushirikiana na sekta binafsi ili kutekeleza adhima ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukuza utalii tiba nchini.

Tayari MOI imeanzisha kliniki kwa ajili ya wagonjwa maalum na kutoka nje ya nchi kwa huduma za kibobezi za tiba ya mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu na kwamba kikao hicho kinalengo la kubainisha maeneo ya ushirikiano.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Mkurugenzi wa MOI Prof. Abeli Makubi na wajumbe wa kamati ya utalii tiba MOI na Mkurugenzi Mkuu wa Global Medcare Bwana Abdulmalik Mollel ambapo kwa pamoja wameanzisha mchakato wa kubainisha maeneo ya ushirikiano yenye lengo la kuharakisha matokeo chanya yanayotarajiwa .

Kwa upande wao Taasisi ya Global Medcare imeipongeza MOI kwa mageuzi makubwa ya uboreshaji wa huduma na miundombinu ndani ya muda mfupi chini ya Prof. Makubi, ikiwa pamoja na uanzishwaji wa Kliniki ya wagonjwa maalum na wa Kimataifa sambamba na maboresho yanayoendelea katika huduma za wagonjwa wa kawaida .

About the Author

You may also like these