Afya check watoa cheti cha shukrani kwa MOI

Na Mwandishi Wetu-MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imekabidhiwa tuzo na kampeni ya Afya Check ya Clouds ya kutambua mchango wake na jitihada kubwa iliyofanya wakati wa kampeni ya Afya Check mkoa wa Dare Saalam.

Tuzo hiyo ya shukurani imekabidhiwa na Mratibu mkuu wa Kampeni hiyo Dkt. Isack Maro na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi

Awali MOI ilishiriki katika kampeni hiyo kwa kutoa madaktari bingwa na wauuguzi ambao walitoa huduma za kitabibu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam bure kuanzia Julai 10 hadi 19, mwaka huu.

About the Author

You may also like these