Walinzi MOI wahimizwa kuboresha huduma kwa wateja, kuwa wavumilivu na kuepuka mita faruko.

Na Mwandishi Wetu-MOI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo (MOI) Prof. Abel Makubi amefanya kikao cha kimkakati na, viongozi wa SUMA-JKT Makao makuu na walinzi wa taasisi hiyo kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi ili kuboresha huduma kwa wateja.

Katika kikao hicho kilichofanyika leo Oktoba, 24, 2023 ukumbi wa MOI mpya Prof. Makubi amewaomba walinzi hao (SUMA JKT) kuwa wavumilivu katika kuwahudumia wagonjwa na ndugu wa wagonjwa ili kuepusha migogoro baina yao kwa sababu eneo la Hospitali linahitaji upendo, huruma na majitoleo.

Pia Mkurugenzi huyo ametoa rai kwa ndugu wa wagonjwa wanaofika MOI kusindikiza au kuwajulia hali wagonjwa kuheshimu miongozo, taratibu na muda wa kuwaona wagonjwa waliolazwa wodini.

“Muda wa kuona wagonjwa ni saa 12 :00 asubuhi hadi saa 1:00 asubuhi, muda wa kuleta chakula ni kuanzia saa 6:30 mchana hadi saa 8: 00 mchana na kuona wagonjwa ni kuanzia saa 10:00 jioni hadi 12:00 jioni na idadi ya watu wanaotakiwa kuingia wodini kumuona mgonjwa ni wawili kwa kupokezana kila baada ya dk 15, tuzingatie hilo” amesema Prof. Makubi. Aidha, walinzi pia wapo kwa ajili ya usalama wa kila mmoja pamoja wa wagonjwa , ndugu zao na mali zao.

Aidha amesema menejimenti inatafakari ombi la wananchi la kutaka kuongezwa kwa idadi ya ndugu wa wagonjwa waliolazwa wanaoruhusiwa kumuona mgonjwa bila kuathiri usalama, afya ya wagonjwa na ndugu zao.

About the Author

You may also like these