Na Abdulaziz Seif-MOI
Watumishi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), leo wamepewa mafunzo maaluma ya kimkakati ya kutoa huduma bora kwa wateja wanaokuja kupata huduma kwenye taasisi hiyo na Benki ya CRDB PLC Makao Makuu jijini Dar es Salaam
Mapema leo asubuhi Mei, 07, 2024 timu ya wataalam kutoka MOI ikiongozwa na Afisa Utumishi Mwandamizi Pezuma Kimale iliwasili makao makuu ya benki ya CRDB PLC kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika tasnia ya huduma kwa wateja.
“Kwa niaba ya Taasisi ya MOI naishukuru Benki ya CRDB kwa kutupa fursa hii ya kujifunza kutoka kwenu, ni imani yangu kuwa mafunzo haya yamefungua milango ya kubadilishana uzoefu baina yetu…niwaahidi kuwa yale tuliyojifunza tutakwenda kuyafanyia kazi” amesema Pezuma
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa CRDB PLC Makao Makuu, Yolanda Urio amesema milango iko wazi kwa Taasisi ya MOI kuendelea kujifunza na kwamba ushirikiano huo ni muhimu katika uboresha huduma kwa wateja.