Viongozi wa MOI wapewa mafunzo ya kimkakati ya uongozi wa kuleta matokeo.

Na Mwandishi wetu- MOI

Viongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wanashiriki mafunzo ya siku 4 ya kimkakati ya uongozi na utawala wenye matokeo ya kuonekana kwa Wananchi, huduma bora kwa wateja na namna ya kukabili msongo wa mawazo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo katika hoteli ya APC Bunju A, Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Laurent Lemery amesema mafunzo hayo ya ni muhimu na ya kimkakati kwa viongozi wote wa MOI na yanalenga kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi kwa kuhakikisha uongozi na usimamizi wa huduma unaleta matokeo ya haraka na ya kuonekana kwa Wananchi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

“ Lengo la mafunzo haya ni kukumbushana namna bora ya kutekeleza malengo tuliyoyapanga kwa kutoa mrejesho, kufanya kazi kwa kuleta matokeo katika huduma kwa wagonjwa na namna bora ya kukabili msongo wa mawazo ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wetu” amesema Dkt. Lemery

Kwa upande wake mtaalam wa huduma bora kwa wateja na Uongozi Padre John Kasembo amewakumbusha viongozi wa MOI kuwa uongozi ni sadaka ambapo kiongozi mzuri lazima awe mfano kwa wale anaowaongoza na kutekeleza kwa vitendo maono ya Taasisi ya Taasisi ya MOI na Taifa.

Naye Meneja Uhusiano Patrick Mvungi ameishukuru Menejimenti ya MOI chini ya Prof Abel Makubi na viongozi wengine kwa kupanga na kuendesha mafunzo hayo ya kimkakati kwa viongozi wote wa MOI yanayozidi kuboresha utendaji na uwajibikaji katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

About the Author

You may also like these