Viongozi MOI wakumbushwa mambo muhimu ya kuzingatia kazini.

Na Mwandishi wetu -MOI Alhamisi Januari 18, 2024

Viongozi wa Taasisi ya tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wakumbushwa kuwa wazalendo, waaminifu, wasikivu, kutoa kauli nzuri na majibu sahihi kwa upole na heshima ili kutoa huduma bora kwa wateja na kujenga uhusiano mzuri baina yao na watumishi waliochini yao.

Hayo yamesemwa leo na Mtaalam wa Masuala ya Utawala na Uongozi John Kasembo katika siku ya pili ya mafunzo ya kimkakati ya uongozi wa kuleta matokeo chanya yanayofanyika katika ukumbi wa APC Bunju A, Dar es Salaam.

“ili kuwa Kiongozi mzuri ni lazima uwe mzalendo, kuitetea nchi yako, wateja wako na Taasisi yako, uwe msikivu, jishushe ili uweze kutoa huduma nzuri na kujenga uhusiano mzuri baina ya wateja na Taasisi, pia unatakiwa utoe kauli nzuri ili kutoa majibu sahihi kwa upole na heshima kwa wafanyakazi waliopo chini yako na wateja unaowahudumia” amesema Kasembo

“Ni muhimu sana kufanya kazi kwa uaminifu, tuepuke kusema uongo na ubazazi kwa wale tunaowaongoza ili waige mfano ulio bora kwa kuwafundisha uaminifu wa maneno na matendo” amesema Kasembo

Pia, Kasembo amesema mabadiliko mazuri ni lazima yawe na utamaduni wenu, mtu akija MOI anajua atapata huduma nzuri na bora kwasababu utamaduni wa MOI ni kutoa huduma nzuri na bora vilevile ni lazima mkague na kufanya tathimi ya mabadiliko mnayoyataka yatokee katika Taasisi yenu.

Naye Mkurugenzi wa huduma za uuguzi MOI Fidelis Minja amesema kiongozi ni lazima uwe na ‘sense of ownership’ ili unavyofanya jambo lolote la Taasisi ulifanye kama lako na uwe wazalendo kwa kuacha ubinafsi na tuwe na utamaduni wa kutunza vizuri vifaa ili vikae muda mrefu.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Takwimu MOI Joshua Ngahyoma amesema wao kama viongozi peke yao hawawezi kuibadilisha MOI ni lazima washirikiane na kila mfanyakazi wa MOI ili kuleta mabadiliko chanya na kuzidi kuboresha huduma kwa wateja.

About the Author

You may also like these