Prof. Makubi: wauguzi tengeni muda wa kuongea na ndugu wa wagonjwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) amewaagiza wauguzi kutenga muda wa kuongea na ndugu wa wagonjwa ili kuwapa mrejesho wa matibabu na maendeleo ya mgonjwa wao.

Rai hiyo ameitoa leo Aprili, 5, 2024 wakati alipokuwa anaongea na watumishi wa kada ya uuguzi ambapo amesisitiza kuwa mawasiliano baina ya wauguzi na ndugu wa wagonjwa yatampunguza malalamiko ndugu hao juu ya kutofahamu mwenendo wa matibabu.

“Ukisikiliza malalamiko mengi ya wananchi yanaonesha hawapati mrejesho wa hali za wagonjwa wao…niwaombe tengeni muda wa kutoa mrejesho kwa ndugu wa wagonjwa, ni muhimu katika kuboresha huduma zetu” amesema Prof. Makubi

Amefafanua kuwa “Kuweni na hari ya kutafuta changamoto ili muzipatie majibu, usisubiri changamoto zikufuate…hakikisheni kila wodi inaweka utaratibu wa kutoa mrejesho kwa ndugu wa wagonjwa”

Mapema Meneja wa Rasiliamali Watu Marry Kayola amesema kikao kazi hicho kimelenga kujadiliana juu ya changamoto za kiutendaji na kuzipatia majibu ili kufanikisha adhima ya taasisi katika kuboresha huduma kwa wateja.

Kwa upande wake Meneja Utawala wa MOI Amir Mkapanda amesema changamoto zote za miundombinu zitapatika ufumbuzi kwa haraka ili kuruhusu utoaji huduma kwa urahisi.

Muuguzi Mbobezi Dorcas Magawa ameushari uongozi kuzipatia majibu changamoto za watumishi ili kukuza hari ya watumishi kutoa huduma bora wa wananchi.

About the Author

You may also like these