MOI yafuturisha watumishi wake


Na Radhia Balozi-MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) ikishirikiana na wadau mbalimbali leo Aprili, 8, 2024 imefturisha watumishi wake waislam walio katika ibada ya funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Lemeri Mchome amesema menejimenti ya MOI kwa mara ya kwanza imeamua kuwafturisha watumishi waislam ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano, umoja na upendo miongoni mwa watumishi.

“Menejimenti ya MOI imeandaa Iftar hii ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono waislam walio katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani…hii ni kwa mara ya kwanza MOI tunafanya tukio kama hili, niwashurkuru wote walioshirikiana nasi katika kufanikisha zoezi hili.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya watumishi wa MOI, Afisa Uhusiano Abdallah Nassoro amesema tukio hilo limeleta faraja kwa waislamu wa Taasisi ya MOI na kwamba wanaishukuru menejimenti kwa kuwajali.

“Kwa niaba ya watumishi wenzangu wa MOI tunaishukuru menejimenti kwa kutuonesha upendo, kutuandalia iftar jambo ambalo limeleta faraja kwa waumini wa dini ya kiisilam” amesema Nassoro

Kwaupande wake Imamu Msaidizi wa Masjid Alrahman Muhimbili Sheikh Mudathir Muhammad amewapongeza menejimenti kwa uwamzi wake huo na kusema kuwa umeacha alama katika utendaji kazi zao.

“Hapa ni kama uchangiaji wa damu salama, tofauti ni kwamba damu huendana na makundi, lakini hapa watu wote wamekula…unapomlisha mtu unakuwa umemchangia damu kwasababu chakula ndo mwanzo wa damu na mwenendo wa matendo yake” amesema Sheikh Muhammad na kuongeza
“Jambo hili ni muhimu sana na linapaswa kuigwa na taasisi zingine…mtu akikuomba msaada wa chakula msaidie kwasababu utakuwa umefanya moja ya jambo kubwa muhimu maishani mwake”
Mwisho

About the Author

You may also like these