Prof Makubi awaagiza wauguzi MOI kuboresha huduma kwa wagonjwa wa ndani na nje

Na Mwandishi wetu-MOI, 28 Juni 2023, Dar es salaam.

Mkurugenzi mtendaji wa MOI Prof.Abel Makubi amewataka wauguzi wa MOI kuboresha huduma kwa wagonjwa mahututi kwa kukaa karibu na wagonjwa kwa kuwa na viti karibu na wagonjwa ili kufuatilia kwa karibu mienendo ya afya zao.

Pia, Prof. Makubi amewaomba wauguzi wa MOI kutoa huduma bora kwa wagonjwa wa ndani na nje kwa kutoa lugha nzuri ,kuepusha wagonjwa kupata vidonda vya ‘pressure’ (Bed sores), kuzuia homa za mapafu hasa (aspiration pneumonia) kuepuka maambukizi (Infections) wodini na kuzuia au kupunguza vifo kwa wagonjwa wandani.

Katika kikao hicho, Prof. Makubi amewalekeza wauguzi kuanza kutumia mfumo wa TEHAMA kuingiza taarifa za wagonjwa baada ya kubaini kwamba baadhi ya wodi hazitumii mfumo huo ambao tayari umesimikwa katika maeneo yate ya kutolea huduma.

Mkutano kati ya Mkurugenzi Mtendaji MOI na Wauguzi

Aidha, Prof. Makubi amewaeleza wauguzi mambo manne ya msingi ambayo yanahitajika kufanyiwa kazi ili kuleta mageuzi makubwa katika utoaji huduma kwa wagonjwa.

‘’Kuna masuala manne ya muhimu ambayo lazima sote tushirikiane ili kuboresha huduma zetu, mambo hayo ni ubora wa huduma, uwajibikaji wa matokeo, kuongeza mapato na huduma kwa wateja (customer care) Alisema Prof. Makubi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi MOI Bw.Fidelis Minja amesema wauguzi wa MOI wako tayari kutekeleza majukumu yao kwa kiwango cha juu ili kufikia malengo ya Taasisi za Serikali.

“Tunashukuru kwa kupata nafasi ya kukutana nawe Mkurugenzi Mtendaji wetu Prof. Makubi, tumekueleza changamoto zetu na tumetoa maoni yetu ya namna ya kuboresha huduma kwa wateja wetu, tunakuahidi ushirikiano wa hali ya juu’’ Alisema Bw.Minja

Nao,wauguzi wa MOI kwa pamoja wamemueleza Prof. Makubi changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja.

About the Author

You may also like these