Maabara

Prof. Makubi aongoza wajumbe wa menejimenti ya MOI kukagua maeneo ya huduma ndani ya hospitali, kusikiliza kero na kutatua changamoto

Na Mwandishi wetu – MOI, Dare Salaam, 01/07/2023

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi leo amewaongoza wajumbe wa Menejimenti ya MOI kupita wodini, wagonjwa wa nje, Idara za uchunguzi , Physiotherapy , maabara, pharmacy na maeneo mengine ya kutolea huduma ili kujionea ubora wa huduma , kusikiliza kero za wagonjwa na ndugu, na kutatua changamoto zilizopo.

Prof. Makubi amesema maeneo ya kutolea huduma ni kipaumbele hivyo ni muhimu changamoto zake zikatatuliwa kwa wakati ili wagonjwa wapate huduma zenye ubora unaotakiwa. ” Naelekeza fedha zozote zinazopatiana ndani ya Hosptali, kipaumbe ni huduma kwa mgonjwa kwanza na kuhakikisha vifaa, vipimo na dawa zipo kila wakati.

Timu ya Menejimenti ya MOI ikifanya ukaguzi wa maeneo ya huduma

“Niwaombe viongozi wenzangu, yale yote tuliyoyaona leo katika maeneo tuliyopitia yafanyiwe kazi kwa wakati” Alisema Prof. Makubi.

Pia Prof. Makubi amelekeza kuviondoa vitanda na Wheelchair zilizochakaa ndani ya wodi , vibadilishwe kwani haviendani na hadhi ya Taasisi ya MOI.

Katika Kitengo cha maabara Prof. Makubi ameomba changamoto zote zilizoibuliwa zitatuliwe kwa wakati ili kuleta ubora wa huduma hasa kuharakisha majibu na yenye viwango vyote vya usahihi.

Mwisho, Prof. Makubi amewashukuru viongozi wote wa MOI kufanya Usimamizi na ufatiliaji wa huduma za wagonjwa siku za weekend , kutatua malalamiko na kukagua mazingira na vifaa kwenye maeneo husika. Aidha , ameelekeza kufanyika clinical audit za ubora wa huduma ndani ya Hospitali kila baada ya siku 14, ikishirikisha top management na watumishi ili kujitathimini na kuendelea kuboresha huduma kila siku..

About the Author

You may also like these