MOI Marathon

Mbio fupi za MOI Marathon msimu wa tatu (3) zafana

Na Mwandishi wetu –
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili MOI imeendesha mbio fupi za MOI Marathon msimu wa tatu kwa lengo la kusaidia walemavu 100 wenye uhitaji wa miguu bandia katika viwanja vya MUHAS ambapo zaidi ya washirki 1300 wameshiriki.

Naibu Katibu mkuu Wizara ya Afya Bi. Grace Maghembe ameipongeza MOI kwa ubunifu na kuanzisha mbio kwaajili ya kusaidia wenye mahitaji maalum.

“Mbio fupi za MOI Marathon ni endelevu ambapo zitawesha walemavu 100 kuendelea na shughuli zao za kila siku hususani katika ujenzi wa taifa.

Matukio ya MOI Marathon 25.06.2023

Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini Prof Mkonyi amesema Mbio za MOI Marathon zitakuwa chanzo cha mapato katika Taasisi ya mifupa MOI kwa lengo la kusaidia wananchi wenye uhitaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi ameishukuru serikali ya awamu Sita kwa kuhakikisha huduma za kibingwa zinapatikana hapa nchini.

Mshiriki wa MOI Marathon Baraka Ali amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kujenga afya na kusaidia watu wenye mahitaji maalumu katika matukio mbalimbali Kama MOI Marathon.

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili MOI inaendelea kutekeleza agizo la serikali ya awamu ya sita kuhakikisha kila mwananchi anapatiwa huduma bora.

About the Author

You may also like these