Watumishi

Watumishi wa MOI wahimizwa kufanya kazi kwa ushirikiano

Na Mwandishi wetu- MOI

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi amewataka watumishi wa MOI kufanya kazi kwa bidii na umoja ili kuleta uwajibikaji na matokeo chanya.

Prof. Makubi amesema hayo katika muendelezo wa vikao baina yake na watumishi wa MOI ambapo leo amefanya kikao na watumishi wa idara ya ICU, HDU, Kitengo cha dharura na kitengo cha dawa za usingizi.

“lazima tutembee kama timu, Taasisi hii ni kubwa na ina maslahi ya nchi, hivyo ili malengo ya wananchi nchi pamoja na Mh. Rais yatimie lazima tufanye kazi kama timu, tukishirikiana naamini tutasonga mbele” Prof. Makubi

Prof. Makubi amewataka watumishi wa MOI kufanya kazi kwa bidii kwa kipindi cha miezi 3 hadi 6 kuanzia sasa ili kuongeza uwajibikaji na mapato.

Kwa upande wao watumishi wa MOI wamemueleza Prof. Makubi changamoto zao pamoja utatuzi wake na kujadili kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mageuzi chanya.

About the Author

You may also like these