Madaktari MOI

Prof. Makubi afanya kikao na madaktari MOI, wamuahidi uwajibikaji

Na Mwandishi wetu-MOI, 16 Juni 2023

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi leo amefanya kikao na madaktari wa MOI kwa lengo la kusikiliza changamoto zao na kujadiliana kwa pamoja namna ya kuboresha huduma , kuimarisha huduma kwa wateja na kuongeza mapato ya Taasisi.

Huu ni muendelezo wa vikao mbalimbali kati ya Prof. Makubi na watumishi wa MOI ili kutafuta majawabu ya changamoto zinazoikabili taasisi ya MOI.

Prof. Makubi amasema ili Taasisi ya MOI ifikie malengo yake lazima kila mtumishi kwa nafasi yake afanye kazi kwa bidii ili kuleta matokeo chanya kwa wagonjwa, Taasisi na Serikali.

“Leo tumekutana hapa ili kujadiliana kwa pamoja namna ya kuboresha huduma, kukumbushana dhana ya uwajibikaji wa matokeo, kuangalia namna bora ya kuongeza mapato ya Taasisi na kuimarisha huduma kwa wateja (Customer care) , hivyo naamini tukiyatekeleza haya tutafikia malengo ya Taasisi yetu” Alisema Prof. Makubi.

Aidha, Prof. Makubi amewakumbusha madaktari wa MOI kujenga utamaduni wa kutoa mrejesho kwa wagonjwa kuhusu matibabu yao ili kuwe na uelewa wa pamoja kati ya mtoa huduma na mteja.

Kwa upande wao madaktari wa MOI wamemueleza Prof. Makubi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utendaji wao wa kila siku na kutoa ushauri wa namna ya kutatu changamoto hizo. Pamoja na mambo mengine madktari wa MOI wameahidi kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ili kufikia malengo ya Taasisi ya MOI ya kuwa Taasisi bora barani Afrika.

About the Author

You may also like these