Na Mwandishi Wetu-MOI, Agusti 25, 2024, Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Prof. Abel Makubi leo amefanya kikao cha kimkakati na madaktari wote wa MOI kwa lengo la kuwapa mrejesho kuhusu mwenendo wa huduma kwa wagonjwa na miradi ya kimkakati inayoendelea.
Akizungumzia suala la huduma ambazo ameelekeza zimeboreka kwa kiasi kikubwa na kuwapongeza sana kwa uwajibikaji wao kwa Wananchi . Prof. Makubi amewaomba madaktari kuendelea kusimamia ubora wa huduma, kupunguza kero za wagonjwa na kutoa mrejesho kwa wagonjwa kuhusu tiba wanayopata, mpango na muendelezo wa matibabu yao
“Niwaombe tena, feedback giving kwa wateja ni kazi yetu sisi madaktari hivyo tunavyopita wodini katika ‘major ward round’ tutumie hata dakika moja kutoa mrejesho kwa wateja wetu ili wawe na uelewa wa kutosha kuhusu huduma tunayowapa, tumetengeneza SOP’S tuzitufuate na kuzitumia kutoa huduma , kuzingatia maadili na kutoa mrejesho” amesema Prof. Makubi.
Akitoa mrejesho kuhusu miradi ya kimakakati Prof. Makubi amesema kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma za MOI kwa wananchi pamoja ongezeko kubwa la wagonjwa, Taasisi ya MOI ina miradi ya kimkakati ya maboresho ya OPD iliyopo na ujenzi wa Jengo la OPD mpya yenye ghorofa tatu na mradi wa Kituo cha utengamao (Rehabilitation centre) katika kiwanja cha MOI kilichopo Mbweni Dar es Salaam. Pia Prof Makubi amewaombwa wataalam hao kujipanga vyema kwa ajili ya kuhudumia AFCON 2027.
Aidha, Mkurugenzi huyo amewaomba madaktari wa MOI kukaa na kujadiliana na kuja na mpango wa kuanza kwa kliniki za siku za mapumziko ili kuongeza wigo wa kuwahudumia watanzania badala ya kwenda kwenye hospitali nyingine ambapo malipo ya kliniki hizo yatafanyika kila mwisho wa mwezi.
Wakitoa maoni yao kuhusu hali ya utoaji huduma na mwenendo wa Taasisi Madaktari wameipongeza manejimenti ya MOI wa mageuzi makubwa inayofanya na kuomba maboresho hayo pia kuendana na masilahi ya watumishi ili kuongeza ari . PROF.MAKUBI AKUTANA NA MADATARI MOI NA KUJADILIANA MWENENDO WA HUDUMA NA MIRADI YA KIMKAKATI INAYOENDELEA MOI
Na Mwandishi Wetu-MOI, Agusti 25, 2024, Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Prof. Abel Makubi leo amefanya kikao cha kimkakati na madaktari wote wa MOI kwa lengo la kuwapa mrejesho kuhusu mwenendo wa huduma kwa wagonjwa na miradi ya kimkakati inayoendelea.
Akizungumzia suala la huduma ambazo ameelekeza zimeboreka kwa kiasi kikubwa na kuwapongeza sana kwa uwajibikaji wao kwa Wananchi . Prof. Makubi amewaomba madaktari kuendelea kusimamia ubora wa huduma, kupunguza kero za wagonjwa na kutoa mrejesho kwa wagonjwa kuhusu tiba wanayopata, mpango na muendelezo wa matibabu yao
“Niwaombe tena, feedback giving kwa wateja ni kazi yetu sisi madaktari hivyo tunavyopita wodini katika ‘major ward round’ tutumie hata dakika moja kutoa mrejesho kwa wateja wetu ili wawe na uelewa wa kutosha kuhusu huduma tunayowapa, tumetengeneza SOP’S tuzitufuate na kuzitumia kutoa huduma , kuzingatia maadili na kutoa mrejesho” amesema Prof. Makubi.
Akitoa mrejesho kuhusu miradi ya kimakakati Prof. Makubi amesema kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma za MOI kwa wananchi pamoja ongezeko kubwa la wagonjwa, Taasisi ya MOI ina miradi ya kimkakati ya maboresho ya OPD iliyopo na ujenzi wa Jengo la OPD mpya yenye ghorofa tatu na mradi wa Kituo cha utengamao (Rehabilitation centre) katika kiwanja cha MOI kilichopo Mbweni Dar es Salaam. Pia Prof Makubi amewaombwa wataalam hao kujipanga vyema kwa ajili ya kuhudumia AFCON 2027.
Aidha, Mkurugenzi huyo amewaomba madaktari wa MOI kukaa na kujadiliana na kuja na mpango wa kuanza kwa kliniki za siku za mapumziko ili kuongeza wigo wa kuwahudumia watanzania badala ya kwenda kwenye hospitali nyingine ambapo malipo ya kliniki hizo yatafanyika kila mwisho wa mwezi.
Wakitoa maoni yao kuhusu hali ya utoaji huduma na mwenendo wa Taasisi Madaktari wameipongeza manejimenti ya MOI wa mageuzi makubwa inayofanya na kuomba maboresho hayo pia kuendana na masilahi ya watumishi ili kuongeza ari .