Upasuaji mpya wa mgongo kwa njia ya matundu (Endoscopic spine surgery) waanzishwa MOI

Na Abdallah Nassoro-MOI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba  ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Prof. Abel Makubi leo Machi, 25, 2024 amefungua Kongamano la 12 la Kimataifa la Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu lililohudhuriwa na washiriki 200 kutoka nchini mbalimbali za Afrika na Marekani, kongamano lililofanyika Jijini Dar es Salaam

Akifungua kongamano hilo lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Weill Cornel cha Marekani kwa kushirikiana na MOI Prof. Makubi amesema uwapo wa kongamano hilo utasaidia kukuza ujuzi wa madaktari wazawa na kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wananchi yenye viwango sawasawa na ile inayopatikana Ulaya, Marekani na Asia.

Amesema kwa sasa Tanzania inakabiliwa na  uhaba mkubwa wa madaktari wa upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu licha ya kuongezeka kwa wagonjwa kunakosababishwa na ajali za barabarani.

“Kwa sasa nchi ina madaktari 23 kati ya hao 13 ni wapo MOI na 10 wapo katika hospitali zingine, madaktari hao hao wanahudumia watanzania 62 milioni” amesema Prof. Makubi na kuongeza, tunashukuru juhudi za Mh. Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu (MB) kwa kwa kuweka kipau mbele kuongeza mafunzo ya kibingwa ma kibobevu katika tasnia hii ambapo zimetengwa Billioni nane na kwa sasa kuna madaktari 14 ambao tayari wapo masomoni.

“Namshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki kwa ustawi wa ushirikiano huu ambapo madaktari na manesi kutoka Tanzania wanakwenda kujifunza Marekani na kujipatia uzoefu kutoka kwa wenzetu. Pia niipongeze wizara ya afya kwa jitihada kubwa za kuboresha sekta ya afya nchini”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upasuaji wa Mgongo kutoka Chuo Kikuu cha Weill Cornel Marekani Prof. Roger Hartl amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha Taasisi ya MOI inakuwa kituo mahiri cha mafunzo, Utafiti na upasuaji wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu Afrika Mashariki na Kati

Mkurugenzi wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu wa MOI Dkt. Lemeri Mchome amesema ushirikiano baina ya MOI na Weill Cornel umewezesha wagonjwa wa mgongo wanaotakiwa kupandikizwa vyuma kutibiwa nchini kinyume na awali ambapo walikuwa wanapewa rufaa kwenda nje ya nchi.

“Miaka 12 ya ushirikiano huu, umefaidika katika tafiti, vifaa tiba na mafunzo…awali tulikuwa tunapeleka wagonjwa nje ya nchi lakini kupitia program hii wagonjwa wote wa mgongo wanatibiwa katika taasisi yetu ya MOI.

Mratibu wa Mafunzo hayo Dkt. Hamisi Shabani amesema mkutano huo umekuja na teknolojia mpya ya upasuaji wa mgongo ambapo mgonjwa ataweza kuruhusiwa kwenda nyumbani siku hiyohiyo au siku inayofuata kutegemeana na maendeleo yake.

Majeruhi wengi wa ajali wanaumia kwenye ubongo na mgongo mafunzo haya ya teknolojia mpya ya kutibu  matatizo ya ubongo na mgongo yatasaidia kuboresha huduma hapa MOI. Ushirikiano huu wa miaka 12 na Weill Cornel umewezesha sisi kama taifa kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa sababu wataalam wetu wamejengewa uwezo wa kutoa tiba sahihi” na poa wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa kununua vipandikizi kupatiwa tiba kupitia mpango huu.

About the Author

You may also like these