Wataalam wa wagonjwa mahututi kutoka MOI waendesha mafunzo katika kanda ya Rufaa Mbeya

Na Mwandishi wetu,
Wauguzi bobezi wa wagonjwa mahututi kutoka Taasisi ya Mifupa MOI watia kambi katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa Mbeya na kuendesha mafunzo ya siku tano ya namna ya kuwahudumia wagonjwa mahututi wenye matatizo ya ubongo na mishipa ya fahamu.

Afisa Uuuguzi bobezi kutoka MOI Bi. Dorcas Magawa amesema hii ni moja ya utekelezaji wito wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Dkt Samia Suluhu Hasan kuhakikisha huduma zinaboreshwa hapa nchini.

“Mafunzo haya yanawashiriki zaidi ya 120 ambapo jopo la wataalamu kutoka Taasisi ya Mifupa MOI waendesha mafunzo ya siku tano kwa nadharia na vitendo kwa lengo la kuongeza ufanisi kwa wauguzi katika kuwahudumia wagonjwa mahututi.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya kanda ya rufaa ya Mbeya Bw. Omari Mchepange amesema ni heshima kubwa kupata mafunzo ya kibingwa na bobezi kutoka kwa wataalam wa MOI kwani ongezeko la ajali na magonjwa ya yasiyoambukizwa kama kiharusi yameongezeka.

Kwa upande wake Dr. Shafii Hamisi daktari wa magonjwa mahututi amesema kuwa mafunzo haya ni endelevu kwani wauguzi wanahitajika kujengewa uwezo ili kuboresha huduma za kiafya hapa nchini hususani katika kuwahudumia wagonjwa mahututi wenye matatizo ya Ubongo na Mishipa ya fahamu.

About the Author

You may also like these