Prof Makubi

Pro.Makubi: Ni Jukumu La Kila Mfanyakazi Kuhakikisha Ubora Wa Huduma Sehemu Za Kazi Hadi Nyumbani


Na Abdulaziz Seifu-MOI
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Prof. Abel Makubi amesema suala la huduma bora kwa wajeta ni jukumu la kila mtoa huduma na kwamba ubora huo unapaswa kuhamia majumbani katika kulea familia.
Prof. Makubi ameyabainisha hay oleo Aprili, 3, 2024 wakati akifungua mafunzo ya mwongozo wa utekelezaji wa njia za S5 na Kaizen katika uimarishaji na uboreshaji wa program zote za ubora kwa atumishi wa MOI.
Amesema ni muhimu kwa washiriki kuboresha utendaji kazi wao ili mafunzo hayo yalete matunda yanayotarajiwa sambamba na kuhamishia mabadiliko hayo katika familia zao ili kuandaa kizazi kinachojali.
“Kila mmoja ahakikishe anabadilika na kutoa huduma bora, mafunzo haya hayatakuwa na maana kama utendaji kazi wetu utabaki palepale” amesema Prof. Makubi
Amesema “Musiishie hapo, maboresho hayo yapelekeni pia na nyumbani ili watoto wet wajifunze kutoa huduma bora wakiwa nyumbani…mafunzo haya yanaziba pengo la kukosekana kwa malezi bora katika ngazi ya familia”
Mapema Meneja wa Udhibiti Ubora na Huduma bora kwa wateja Dkt. Paul Kazungu amesema mafunzo hayo ya siku tatu yamelenga kuwajengea uwezo washiriki wa kutoa huduma bora kwa wateja.
“Kitego chetu kitaendelea kuwajengea uwezo watoa huduma wetu ili kuhakikisha jukumu la kuboresha huduma linatekelezwa na kila mmoja wetu” amesema Dkt. Kazungu

About the Author

You may also like these