MOI yapokea msaada wa Vifaa tiba na mahitaji kutoka kampuni ya CUSNA

Na Mwandishi wetu- MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imepokea msaada wa vifaa tiba kutoka Kampuni ya usafirishaji ya CUSNA Investment kwaajili ya kuboresha zaidi utoaji wa huduma MOI na kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji.

Vifaa tiba hivyo vimepokelewa leo Alhamisi Desemba, 21, 2023 na mkurugenzi wa huduma za upasuaji wa ubongo na mgongo Dkt. Lemery Mchome ambaye ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada wa vifaa hivyo.

“Napenda kushukuru kwa niaba ya Menejimenti ya MOI inayoongozwa na Prof. Abel Makubi kwa vifaa tiba hivi ikiwemo machera, viti mwendo, viti vya kukusanyia damu pamoja na vyakula, mafuta ya kupikia na viti vya watoto ambavyo vitaboresha zaidi utoaji wa huduma zetu na zitawasidia wagonjwa wenye uhitaji” amesema Dkt. Mchome

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya CUSNA Investment Herry John amesema kuwa ni utamaduni wao kila mwisho wa mwaka kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji kwa kuwapa vifaa tiba na mahitaji mengine.

Naye Meneja wa Ustawi wa Jamii Bw. Jumaa Almas ameishukuru Kampuni ya CUSNA investment kwa msaada waliotoa MOI na amewaomba wadau wengine wazidi kujitokeza kwa wingi kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji maalum.

About the Author

You may also like these