Mbunge awapongeza madaktari na Wauguzi MOI

Na Mwandishi Wetu, MOI

Mbunge wa Viti Maalum kutoka Zanzibar Mhe: Asha Juma, maarufu Mama Mshua amewashukuru na kuwapongeza Madaktari na Wauguzi wa Taaasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kwa kutoa huduma bora na kwa wakati katika kipindi ambacho alilazwa hospitalini hapo kwa matibabu baada ya kuvunjika kwa mfupa wa paja la kulia.

Akizungumza hospitalini hapo Desemba, 27, 2023 Mama Mshua amesema madaktari na wauguzi hospitalini hapo walimpokea na kumfanyia upasuaji kwa upendo wa hali ya juu ndani ya muda mfupi, jambo ambalo amesema limemtia faraja.

“Nikiwa Kigali Rwanda kwenye michezo ya Mabunge, nilitereza nikaanguka, nilivunjika mfupa wa paja, nilipatiwa huduma ya kwanza kule na kisha kukimbizwa hadi MOI ambako nilipokelewa na kupatiwa matibabu kwa haraka sana” anahadhia Mbunge huyo na kuongeza

“Ndani ya siku 11 tangu nipate ajali, naweza kuchupa-chupa mwenyewe, kwakweli naipongeza MOI, naipongeza Wizara ya Afya na nampongeza Mhe:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha sekta ya afya…

MOI wanatoa huduma nzuri sana, kama kuna mahitaji yeyote ili kuboresha zaidi, niiombe wizara isisite kutuletea bungeni nasi tutaipitisha ili huduma hizi ziboreshwe zaidi kwa maslahi ya Watanzania”

About the Author

You may also like these