MOI kuwa kituo cha mafunzo endelevu kwa mabingwa wa upasuaji wa ubongo Afrika.

Na Mwandishi Wetu-MOI

Jumuiya ya madaktari bingwa wabobezi wa upasuaji wa ubongo ya umoja wa Ulaya -European Association of Neurosurgical Societies (EANS )imependekeza Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kuwa kituo chao cha umahiri barani Afrika kwa ajili ya upasuaji wa kibobezi wa ubongo na kutoa mafunzo na kwa watalaamu wanaotoka nchi zingine. .

Akiongea wakati wa kuhitimisha kambi ya mafunzo maalum ya vitendo kwenye upasuaji wa Ubongo, Mkufunzi kutoka EANS Dkt. Petr Ondra amesema kuwa wamedhamiria MOI kuwa kituo cha umahiri wa mafunzo hayo baada ya kuridhishwa na watalaamu waliopo na uwekezaji wa vifaa vya kisasa uliofanywa na Serikali.

Mwenyekiti huyo akiwa na madaktari bingwa wabobezi wa upasuaji wa Ubongo kutoka Mataifa 12 duniani walipiga kambi ya siku tano MOI wakitoa mafunzo ya nadharia na vitendo vya upasuaji wa Ubongo ambapo wamehitimisha leo Ijumaa Novemba 24, 2023 ambapo jumla ya wagonjwa 10 walifanyiwa upasuaji wa ubongo.

Ombi hilo limekubaliwa na menejimenti ya MOI chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake Prof Abel Makubi ambaye amewahakikishia wataalam na wakufunzi wabobezi kutoka jumuiya hiyo kuwa MOI ina mazingira wezeshi ya kufanyia mafunzo hayo na pia inawataalam wa kushirikiana nao na teknolojia ya kisasa

Pia Prof. Makubi amesisitiza kuwa mafunzo haya yanaendana na sera za Wizaraya Afya, pia huduma ya utalii tiba itayopelekea wagonjwa kutoka mataifa mbalimbali kuja MOI kupata huduma za matibabu ya Ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.

Chini ya mpango huo EANS itatoa madule mbambali za upasuaji wa ubongo kupitia taasisi hiyo ambapo watalaamu wa Afrika watatakiwa kufika MOI badala ya kwenda nchi za ulaya.

About the Author

You may also like these