Wiki ya utoaji wa huduma; Wataalam MOI wahimizwa kutoa mrejesho na mpango wa matibabu kwa wagonjwa.

Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja Madaktari wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wamehimizwa kutenga muda zaidi wa kutoa mrejesho kwa wagonjwa kuhusu tiba , mpango mzima wa matibabu na kupunguza mlolongo wa kupata huduma ili kuishi dhana ya huduma Bora kwa wateja.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi amebainisha hayo leo Alhamisi Oktoba 5, 2023 akizungumza na wataalam, Wagonjwa na ndugu wa Wagonjwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

“Tafsiri ya kupata huduma kwa wagonjwa si kupewa dawa na kufanyiwa operation tu , bali ni kuanzia kupokelewa , kuonwa na doctors kwa kuchukuliwa maelezo , kufanyiwa vipimo , kupewa mrejesho , kupata huduma za uuguzi na hatimaye kupewa dawa , au upasuaji au vyote” amesema Prof. Makubi

About the Author

You may also like these