Watumishi TPA wawafariji watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi MOI

Erick Dilli- MOI

Watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Idara ya Masoko na Uhusiano kwa Umma wametembelea wodi ya watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopata matibabu katika hospitali ya MOI.

Tukio hilo limefanyika leo Ijumaa tarehe 24, Januari 2025, ambapo Afisa Masoko Mkuu wa TPA, Ally Mayai Tembele amesema huwa ni utaratibu wao kila mwaka kufanya matendo hayo ya faraja kwa watu wenye mahitaji maalum na leo wameamua watembelee MOI kwa watoto wenye changamoto ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.

“Tumechagua kutembelea watoto hawa wenye changamoto ya kichwa kikubwa na mgongo wazi kwa lengo la kuwapa faraja wakati wakipatiwa matibabu na tumefanikiwa kuja na baadhi ya vitu (Mafuta, Sabuni, Nepi za watoto na wakubwa) pamoja na kulipia sehemu ya matibabu ” amesema Bw. Ally

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii wa MOI, Anitha Minja amewashukuru wadau hao kutoka TPA kwa moyo wao wakujitoa na kutoa rai kwa wadau wengine kujitokeza kutoa msaada.

“Tunashukuru wadau wetu kutoka TPA kwa moyo wao na kuwapa tabasamu watoto hawa wenye changamoto ya kichwa kikubwa na ninaomba kwa wadau wengine kujitokeza kwa wingi ili kutoa msaada” amesema Bi. Anitha

About the Author

You may also like these