MOI yanadi tiba utalii katika mkutano wa nishati wa wakuu wa nchi za Afrika.

Na Mwandishi wetu- Dar es Salam.

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imenadi fursa ya tiba utalii iliyopo nchini katika mkutano wa wakuu wa nishati wa wakuu wa nchi za Afrika ulioanza Januari 27 na kufikia tamati 28/01/2028 katika ukumbi wa kimataifa Mwalimu Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.

Akizungunza na washiriki na viongozi mbalimbali waliotembelea banda la MOI daktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo na Mgongo MOI Dkt. Aingaya Kaale amewaalika viongozi hao kuwaleta wagonjwa Tanzania

“Serikali yetu imefanya uwekezaji mkubwa kwenye taasisi yetu ya MOI, tunavyo vifaa tiba vya kisasa, wataalam wabobezi pamoja na miundombunu bora inayotuwezesha kutoa huduma za kibingwa za viwango vya kimataifa “ Alisema Dkt. Kaale

Alisema, hivi sasa Taasisi ya MOI inatoa huduma za kibingwa na kibobezi za upandikizaji nyonga na magoti, upasuaji tata wa mgongo, upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo, upasuaji wa mivunjiko ya mifupa yote, upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu, tiba ya maumivu sugu , upasuaji na uchunguzi wa ubongo bila kufungua fuvu na upasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo.

Aliongeza kwamba Taasisi ya MOI imeendelea kutambulika na kupata ithibati ya kimataifa ya huduma bora kutoka Taasisi na Jumuiya mbalimbali za kimataifa ikiwemo AO alliance/AO Trauma, COSECSA na ithibati ya maabara ya SADCAS.

Kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewezesha Taasisi ya MOI kutoa huduma kwa wagonjwa kutoka mataifa ya Comoro, Malawi, Zambia, Zimbabwe na mataifa mengine barani Afrika.

About the Author

You may also like these