vichwa vikubwa

watoto 25 wafanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa na mgongo wazi katika kambi maalum

Na Mwandishi wetu- MOI

Watoto 25 wenye vichwa vikubwana mgongo wazi wamefanyiwa upasuaji katika kambi maalum iliyofanyika leo katika taasisi ya MOI.

Daktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu wa MOI Dkt. Hamis Shabani amesema wamefanya kambi maalum ya upasuaji wa watoto 25 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi kutokana na ushirikiano mkubwa kati ya Taasisi ya MOI na wadau wake katika kukabiliana na idadi kubwa ya watoto wanaohitaji upasuaji .

“Leo tumefanikiwa kuwafanyia upasuaji watoto 25 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ambapo wanne kati yao walikuwa na kichwa kikubwa pamoja na mgongo wazi na hali zao zimeimarika” amesema Dkt. Shaban.

Naye mtaalam wa kutoa dawa za usingizi, Juma Said ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwezeka katika sekta ya afya hususani MOI ambapo kupitia uwekezaji huo wamefanikiwa kuendelea kutoa huduma za kibingwa kwa wagonjwa.

Taasisi ya MOI imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali katika kuendesha kambi za upasuaji na kutoa elimu kwa wataalam wa Afya kwa lengo la kuhakikisha wanatoa matibabu kwa watoto wote wenye tatizo hilo.

About the Author

You may also like these