Wanawake tughe MOI washauriwa kujiunga na mfuko wa uwekezaji wa hati fungani wa utt amis

Na Amani Nsello- MOI

Wanachama Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania tawi la Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (WANAWAKE TUGHE MOI) wameshauriwa kujiunga na Mfuko wa Uwekezaji wa UTT Amis.

Ushauri huo umetolewa jana Ijumaa Desemba 20, 2024 na Afisa Masoko, Rebecca Nyanda kutoka Kampuni ya UTT Amis wakati akiwasilisha mada ya Faida ya Uwekezaji wa Hatifungani (BOND Fund) katika Mkutano wa Wanawake wa TUGHE tawi la MOI.

“Nawashauri wanawake wenzangu mjiunge na mfuko huu wa uwekezaji, ukiwa na kiasi cha milioni 10 za Kitanzania unaweza kuwekeza, kupitia mfuko huu utaweza kukuza mtaji na kila mwezi utakuwa unapokea gawio, na hilo gawio lako litakuwaconnected moja kwa moja na akaunti yako ya benki”-amesema Bi. Rebecca

Awali akifungua mkutano huo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Meneja Usafi na Ufuaji, Elizabeth Mbaga amewaasa wanawake kuwa na mipango ili waweze kuwekeza na kukuza mitaji yao, hiyo itawasaidia hata baada ya kustaafu.

“Nawaomba muwe na mipango, mkiwa na mipango itakuwa rahisi kwenu kuwekeza na kukuza mitaji yenu… Lakini mkisema muwekeze tu bila mipango itakuwa sawa na bure”- amesema Bi. na kuongeza

” Muendelee kupendana na kushikamana na niwaahidi tutazifanyia kazi changamoto zenu zote kwa kushirikiana na viongozi wenu wa Wanawake wa TUGHE MOI”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wanawake TUGHE MOI, Elizabeth Mrindoko amewashukuru wanawake hao wa Taasisi ya MOI kwa kuhudhuria mkutano huo na kuwaasa kufanyia kazi yale yote waliyoelezwa katika mkutano huo hususani wa kuwekeza katika Mfuko wa Hatifungani wa UTT Amis

About the Author

You may also like these