Nyonga Zanzibar

Wagonjwa 16 wapandikizwa nyonga na goti bandia Zanzibar

Na Mwandishi wetu – Zanzibar, 07 Julai 2023

Taasisi ya tiba ya Mifupa Muhimbili MOI kwa kushirikiana na hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar zimeendesha kambi maalum ya upasuaji wa kupandikiza goti na nyonga bandia ambapo zaidi ya wagonjwa 16 wamefanyiwa upasuaji katika kpindi cha siku tano.

Kambi hiyo imefanyika ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano kati ya Hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja na Taasisi ya MOI wenye lengo la kusogeza huduma za kibingwa na kibobezi karibu na wananchi.

Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Nassor Mazrui amesema kambi hii ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ally Mwinyi la kuhkikisha wananchi wanapata huduma za kibingwa na kibobezi bila kulazimika kuzifuata huduma hizo Dar es Salaam au nje ya nchi.

“Leo ni siku ya pekee kwani tumekutana hapa kueleza matunda ya ushirikiano kati ya Hospitali yetu ya Manzi Mmoja na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili-MOI, kama mnavyofahamu mwezi novemba mwaka jana ushirikiano huu ulianza na leo tunashuhudia matunda yake ambapo madaktari bingwa na wauguzi kutoka MOI wamekuja hapa Zanzibar kuwahudumia wananchi wetu” Alisema Mhe. Mazrui.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Dkt.Muhiddin Mahmoud amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe Dkt Hussein Mwinyi pamoja na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui kwa usimamizi imara kwenye sekta ya Afya.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Violet Lupondo amesema Taasisi ya MOI imekua ikitekeleza kwa vitendo agizo la Serikali la kuhakikisha huduma za kibingwa za MOI zinasogezwa karibu na wananchi ambapo kwa sasa huduma hizo zinapatikana katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuwapunguzi wananchi usumbufu wa kufuata huduma MOI Dar es Salaam.

About the Author

You may also like these