Upasuaji kwa njia ya matundu ya pua

Upasuaji kwa njia ya kisasa

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imeanza kutumia mbinu mpya ya kuondoa uvimbe katika sakafu ya Ubongo kupitia tundu la pua ambapo wagonjwa 10 walifanyiwa upasuaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema huduma hii mpya na ya kisasa inaufanisi mkubwa kwenye tiba kwani muda wa kufanya upasuaji ni mdogo na muda wa mgonjwa kukaa hospitali ni mfupi pia.

“Madaktari wetu wanafundishwa mbinu hii na mtaalamu wetu kutoka Uganda ambayeni zao la MOI, mtaalamu huyu alisoma MOI akaenda kujifunza zaidi nchini India na Marekani ambapo amepata ujuzi zaidi na amerudisha ujuzi huo nyumbani” Alisema Dkt. Respicious Boniface

Kwa upande wake Daktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu MOI Dkt. Aingaya Kaale alisema upasuaji huo unatumia njia rahisi, salama zaidi ambapo inachukua saa moja mpaka mawili na mgonjwa anakaa wodini siku chache anaruhusiwa kwenda nyumbani.

Kwa upande wa Daktari mbobezi wa upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya fahamu wa Uganda Dkt. Blessing Michael alisema amekuja MOI kuwafundisha Madaktari wenzake njia ya kisasa ya upasuaji huo ambao alijifunza Ulaya kwani kwa kutumia njia hiyo mgonjwa anapona haraka zaidi.

Mkazi wa Temeke, Ramadhan Msuya aliishukuru Serikali kwa kuhakikisha huduma bora za kibingwa zinapatikana hapa nchini ambapo watanzania wengi wanaweza kupata huduma hizo.

About the Author

You may also like these