Mkuu wa WIlaya ya Temeke Mh. Jokate Mwegelo

MOI yazindua huduma mpya

Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh. Jokate Mwegelo alizindua huduma mpya ya kliniki jongefu katika hospitali ya Mbagala ambapo zaidi ya wagonjwa 400 walihudumiwa na madaktari bingwa wa MOI.

Mhe. Mwegelo alipongeza uongozi wa MOI kwa kubuni na kuanzisha huduma hii ya ya kusogeza huduma za kibingwa za mifupa, mgongo na mishipa ya fahamu kwa wakazi wa Wilaya ya Temeke.

“Ahsanteni kwa kuamua kuzindua huduma hii muhimu katika hospitali yetu ya Mbagala Rangi tatu, kwa namna ya pekee nimshukuru Mkurugenzi Mtendajiwa MOI Dkt. Respicious Boniface kwa kweli mnafanya kazi kubwa na utendaji wenu unaonekana hususani kwenye hili la kuongeza huduma kwa wananchi.” Alisema Mhe. Mwegelo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Samuel Swai alisema wataalamu wa MOI watakuwa wakizunguka katika vituo mbalimbali vya afya mikoani Dar es Salaam kutoa huduma za kibobezi zinazotolewa na taasisi ili kuwapatia huduma wananchi.

“Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwenye Taasisi yetu, hivi sasa tunavyo vifaa vya kisasa na wataalamu wengi hivyo tumeona ni vyema tusogeze huduma kwa wananchi”  alisema Dkt. Swai.

Kwa upande mkazi wa Mbagala Rangi tatu Fatma Mgimbu aliipongeza MOI kwa kuwasogezea huduma za kibingwa na hivyo kuwaondolea adha ya kuzifuata huduma hizo MOI.

About the Author

You may also like these