Menejimenti na wafanyakazi wa Taasisi ya tiba ya mifupa na ubongo Muhimbili (MOI) wamempa tuzo ya shukrani aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi kwa mageuzi makubwa aliyoyafanya katika Taasisi hiyo kwa kipindi cha muda mfupi wa miezi 11.
Tuzo hiyo imetolewa leo MOI kwenye hafla fupi ya kumuaga Prof. Makubi ambaye ameteuliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma.